Mtazamo wa al-Khaliyliy juu ya maneno Allaah aliyozungumza na Mitume Wake

Halafu al-Khaliyliy akataka kuwapaka mchanga wa machoni na kuyafasiri maneno ya Allaah pamoja Manabii na Mitume Wake kama mfano wa maneno Yake (Ta´ala):

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Na bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno ya kwelikweli.”[1]

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ

”Alipokuja Muusa katika muda na pahala pa miadi Yetu na Mola wake akamzungumzisha.”[2]

Maneno yote ambayo Allaah amezungumza na viumbe Wake ya kwamba kuzungumza kwa Allaah ni kuzua maneno katika kipindi hicho na maana ya kuzua ni kuumba maneno. Hakutofautishi kati ya yale maneno ya Allaah anayozungumza pale anapotaka na vile anavotaka ambayo yamesimama kwenye dhati ya Allaah na aina hiyo kama Tawraat, Injiyl, az-Zabuur, suhufi za Ibraahiym na Muusa na Qur-aan na yale maneno yote anayozumgumza Allaah kwa matakwa na utashi Wake.

[1] 04:164

[2] 07:143

  • Mhusika: Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 128-129
  • Imechapishwa: 08/04/2017