Mtazamo wa Ahl-us-Sunnah juu ya mambo ya ghaibu

Kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah ni kwamba mambo yaliyofichikana mlango wake ni mmoja: nao ni kuwa wanajisalimisha kwa kila andiko pasi na kuingia ndani katika uhakika wa maana yake. Mambo yaliyofichikana wanajisalimisha kwayo kwa udhahiri wa maana ambayo imefahamishwa na andiko hilo. Ama kuhusu ujuzi wa uhakika wa hali hizo wanamwachia Allaah kwa sababu ni mambo yaliyofichikana.

Yale yote ambayo yameelezewa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mambo ambayo hatujayaona, sawa katika yale mambo ambayo yatakuwa karibu, baina ya mauti ya kila mja mpaka Qiyaamah kifike, yatayokuwa katika uwanja wa Qiyaamah na siku ya Qiyaamah, yote hayo mlango wao ni mmoja: wanajisalimisha kwayo na kuyathibitisha kama yalivyokuja. Hawayaingilii kwa kuyafasiri kimakosa na kuyapotosha. Haya ni kutokamana na kwamba ni wajibu kwa waja kuamini udhahiri wa matamko na udhahiri wa dalili. Wasiyaingilie kwa kuzipindua dalili kinyume na inavyoonesha udhahiri wake. Asli ya maneno ni uhakika.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 117
  • Imechapishwa: 28/08/2020