Mtawala na si wewe mwenye kubomoa makaburi


Swali: Inatokea wakati mwingine kunakuwa hakuna mtawala kwa muda mrefu kwa sababu ya mapinduzi. Inachukua muda mpaka kuwekwe mtawala. Inajuzu kubomoa makuba au makaburi katika kipindi cha muda huu?

Jibu: Hapana. Ukiyabomoa watajenga mazuri zaidi kuliko yale yaliyokuweko. Mtawala ndiye anatakiwa kuwakataza, si wewe. Hakuna yeyote awezae kupinzana na mtawala tofauti na wewe ambaye huenda hata wakakuua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (59) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16543
  • Imechapishwa: 18/09/2017