Swali: Ni lazima kwa ummah wote kula kiapo kwa mtawala na unasemaje juu ya mtu ambaye anahoji juu ya mtawala asiyehukumu kwa Shari´ah asilimia kwa mia?

Jibu: Simjui ni nani huyu muulizaji. Je, yeye ni katika Ahl-ul-Hall wal-´Aqd[1] ili aulize swali kama hili? Je, watawala wa Banuu Umayyah wote walihukumu kwa Shari´ah katika kila kitu? Je, makhaliyfah wa Banuul-´Abbaas walifanya hivo? Je, wanachuoni waliokuweko kipindi hicho katika Taabi´uun, Maswahabah wa mwisho, waliokuja baada ya Taabi´uun, rika la ash-Shaafi´iy na rila la Ahmad bin Hanbal walifanya uasi dhidi ya yeyote? Bali walikuwa wakiwanasihi watu. Ni lazima kwa mtu kusikiliza na kutii katika yale aliyoyaridhia na katika yale asiyoyaridhia muda wa kuwa yeye hakuamrishwa kufanya maasi. Kuhusu kitendo cha mtawala yeye kufanya maasi, basi itambulike kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mpaka muone kufuru ya wazi ambayo kwayo mko na dalili kutoka kwa Allaah.”

Bi maana isiwe ni kufuru yenye kutatiza. Mtu anatakiwa kuwa mwangalifu juu ya upotofu na kuteleza juu ya swali kama hili.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-kina-nani-ahl-ul-hall-wal-aqd-wanaomteau-mtawala/

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqat-ul-Bay´ah fiyl-Islaam wa Bayaan Shuruutwihaa wa Khatwar Naz´ihaa
  • Imechapishwa: 04/12/2020