Mswaliji mmoja na imamu – watapanga safu vipi?

Lau watu wawili wataswali watasimama sawa au imamu atasogea mbele kidogo? Watasimama sawa na hakuna ambaye atasogea mbele ya mwenzake. Mmoja kusogea mbele ya mwenzake ni jambo linaenda kinyume na Sunnah. Sunnah ni kwa watu wawili waliosimama safu moja wasimame sawa. Hii ndio Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (16)
  • Imechapishwa: 19/11/2017