Swali: Mtu ambaye amekuja amechelewa akiswali pamoja na imamu. Wakati imamu alipoleta Tasliym mtu huyo akasimama kukamilisha swalah yake ambapo imamu akasujudu sijda ya kusahau baada ya kumaliza kutoa Tasliym. Mtu huyo arudi au afanye nini?

Jibu: Afanye kama ambavo endapo angesimama pasi na kusoma Tashahhud ya kwanza. Kama hajasimama kwa kunyooka basi anatakiwa kurudi nyuma. Kama amekwishasimama kwa kunyooka basi anatakiwa kuendelea na swalah yake na mwishoni mwa swalah yake atasujudu sijda ya kusahau.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 19/02/2021