Mswaliji anasema ´Tumeomba msaada kwa Allaah` nyuma ya imamu

Swali: Baadhi ya waswaliji pindi kunaposomwa:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Hakika Wewe pekee ndiye tunakuabudu na Wewe pekee tunakuomba msaada.”[1]

Husema:

استعنا بالله

“Tumeomba msaada kwa Allaah.”

Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah kwa maamuma ni wao kunyamaza kwa ajili ya imamu wao. Akimaliza al-Faatihah imamu aitikie “Aamiyn” na waswaliji pia waitikie “Aamiyn”. Aamiyn hii inamtosheleza na mtu kila kitu anachosema wakati imamu anaposoma al-Faatihah.

[1] 01:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 318
  • Imechapishwa: 09/05/2020