Swali: Inajuzu kumpa mtu aliekusomea Ruqyah kiwango fulani cha mali cha kisomo hichi?

Jibu: Hili ni jambo linalojuzu. Kwa dalili ya Hadiyth ya Ruqyah ya Maswahabah, pindi walipomsomea Labiyd na wakachukua mnyama. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ambacho kina haki zaidi kukichukulia ujira, ni Kitabu cha Allaah.”

Hili ni jambo linalojuzu, lakini kuacha (kuchukua ujira huo) ni bora. Lakini akihitajia (ujira huo), hakuna neno. Pamoja na kuwa, haitakikani kwake (msomaji) kufanya hii ndo ikawa pupa (hamu) yake kubwa na chanzo cha chumo lake. Lakini lau tuchukulie kamsomea mtu, akampatia kitu (katika mali) au (msomaji) akamuwekea sharti ya kumpa, haina neno. Kwa sharti asichukulie hii ndo ikawa pato na chumo lake (la kila siku).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=nA9SNO7PK30
  • Imechapishwa: 19/03/2018