Msomaji wa kiume kumgusa mwanamke wakati wa matabano

Swali: Ni ipi hukumu ya msomaji kugusa paji la uso la mwanamke anayemsomea katikati ya kisomo kwa ajili ya kumtibu kutokamana na uchawi?

Jibu: Akiwa ni mwanamke wa kando naye haijuzu kwake kumgusa. Ama akiwa ni katika Mahram zake hakuna ubaya. Lakini mwanamke wa kando asimguse. Amsomee bila ya kumgusa. Hakuna haja ya kugusa. Asimguse mwanamke wa kando; si paji lake la uso, mkono wake wala kichwa chake.

Muulizaji: Mwanamke huyo amuonyeshe sehemu ya kichwa au nywele?

Jibu: Asimuonyeshe. Amtemee cheche za mate bila ya kumgusa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/39/%D9%84%D8%A7-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D9%84%D9%84%D8%B1%D8%A7%D9%82%D9%8A-%D9%84%D9%85%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A3%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%A3%D8%AC%D9%86%D8%A8%D9%8A%D8%A9-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D9%82%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 26/01/2020