Swali: Mshiriki wangu wa biashara alinipa pesa ili ninunue bidhaa fulani. Kabla ya kufanya kazi hiyo zikaibiwa pesa hizo ndani ya gari yangu pasi na kufanya uzembe katika hilo. Ni ipi hukumu?

Jibu: Alikwamini umnunulie gari na pesa zikaibiwa pasi na kuzembea. Hakuna kinachokulazimu, kwa sababu amekuamini katika jambo hilo na wewe hukufanya uzembe. Huu ni ugomvi. Pengine madai haya yakakanushwa na huyo mwengine… Wanatakiwa kutatua jambo hili mahakamani. Baadhi ya watu wanapindua uhakika wa mambo ili ujibu vile wanavotaka wao. Kisha baadaye wanaenda na kusema fulani amesema hivi na hivi. Msituulize juu ya magomvi yanayotokea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 19/02/2022