Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote yule anayemsitiri muislamu, basi Allaah atamsitiri hapa duniani na Aakhirah.”

Hili linahusu waislamu wote, sawa ikiwa ni wema na wachaji Allaah au ni watenda dhambi. Kumsitiri muislamu ni katika matendo bora. Bali kuna kikosi cha wanachuoni wanaonelea kuwa ni wajibu. Muislamu ambaye hana uwezo wa kuamrisha mema na kukataza maovu, ni wajibu kwake kumsitiri ndugu yake muislamu au ahimize hilo. Ikiwa kuna maasi anayoyajua kwake anayanyamazia. Akijua mapungufu kutoka kwake anayanyamazia na wakati huohuo anajitahidi kumnasihi na kumuokoa nayo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 496
  • Imechapishwa: 10/05/2020