Msingi wa vitu vyote ni kufaa na maana tatu za neno اسْتَوَى

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Yeye ndiye ambaye amekuumbieni yote yaliyomo ardhini kisha akazielekea mbingu na akazitimiza mbingu saba. Naye juu ya kila jambo ni Mjuzi.”[1]

Kwa ajili ya kukufanyieni wema na huruma amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini ili muweze kunufaika navyo, kuburudika na kupata mazingatio kwavyo.

Aayah hii tukufu inajulisha kwamba msingi wa vitu ni uhalali na usafi. Kunatoka ndani yake vile vitu vichafu. Uharamu wavyo unachukuliwa kupitia Aayah hiihii na utambuzi wa malengo yavyo. Jengine ni kwamba Allaah ameviumba vitu hivyo kwa ajili vitunufaisha sisi. Kunaondoka ndani yake vile vitu vyenye madhara. Miongoni mwa ukamilifu wa neema Zake ametukataza vitu vichafu kwa ajili apate kututakasa. Maneno Yake:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ

“… kisha akazikusudia mbingu na akazitimiza mbingu saba. Naye juu ya kila jambo ni Mjuzi.”[2]

Neno اسْتَوَى linakuja ndani ya Qur-aan likiwa na maana tatu:

1 – Wakati fulani linakuja kama lilivyo. Linakuwa na maana ya ukamilifu na utimilifu. Ni kama mfano wa pale aliposema kuhusu Muusa:

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا

“Alipofikia umri wa kupevuka na akaimarika kikamilifu, basi Tulimpa hekima na elimu.”[3]

2 – Maana nyingine linakuja likiwa na maana ya kuwa juu. Hapo ni pale linapofuatishiwa baada yake na على. Kama mfano wa maneno Yake (Ta´ala):

ثم استوى على العرش

“Kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[4]

لِتَسْتَوُوا عَلَى ظُهُورِهِ

”Ili mlingamane sawasawa juu ya mgongo wake… “[5]

3 – Maana nyingine linakuja kwa maana ya kukusudia. Hapo ni pale ambapo litakuja baada ya إلى , kama ilivyokuja katika Aayah hii. Ikiwa na maana kwamba Allaah alipomaliza kuziumba ardhi alikusudia kuziumba mbingu na akazifanya kuwa mbingu saba ambapo akaziumba, akazimairi na kuzisanifu.

يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا

“Anajua yale yanayoingia ardhini, na yale yatokayo ndani yake, na yale yanayoshuka kutoka mbinguni, na yale yanayopanda ndani yake.”[6]

يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ

“Anayajua yale wayafichayo na wanayoyadhihirisha.”[7]

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ

“Kwani hajui Yule aliyeumba na hali Yeye ni Mwenye kuendesha mambo kwa upole, Mwenye khabari zote?”[8]?

Anajua yasiri na yaliyofichikana.

[1] 02:29

[2] 02:29

[3] 28:14

[4] 07:45

[5] 43:13

[6] 57:04

[7] 64:04

[8] 67:14

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Mandhwumah al-Haaiyyah
  • Imechapishwa: 25/05/2022