Miongoni mwa alama za Tahazzub yenye kusemwa vibaya ni kupenda na kuchukia mseto. Bi maana kupenda kuwe kumefupika na fikira, mtu na mfano wa hayo. Wafuasi wakimfanya mtu kuwa ndiye kunapendwa na kunachukiwa kwa ajili yake na kule anakoelekea ndiko wanakoelekea. Kwa msemo mwingine wakamfanya yeye kuwa ndio msingi na wakayapokea ya wengine pale tu yatapokuwa ni yenye kuendana na msingi wa mtu huu na vinginevyo maneno yake yatakuwa ni yenye kurudishwa na si yenye kukubaliwa. Huu ndio Tahazzub iliyosemwa vibaya na Allaah kwa kuwa Allaah amewajibisha kuwapenda waumini wote kwa kiwango cha dini na utiifu wao. Amesema Shaykh-ul-Islaam katika “Bughyat-ul-Murtaad”:

“Kuhusu waumini na watawala – katika wanachuoni na viongozi na wale Mashaykh na wafalme wanaoingia humo – wana haki kwa kiasi cha ile dini waliyosimama nayo. Wanatakiwa kutiiwa katika kumtii Allaah na ni wajibu kupewa nasaha na kusaidiwa katika wema, uchaji Allaah na mengineyo ambayo ni haki vilevile kwa waumini wengine katika kupewa nasaha, kupendwa na haki nyenginezo zilizotolewa dalili na Qur-aan na Sunnah.”

Amesema tena Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah):

“Atakayemfanya mtu – yeyote awaye – kwa njia ya kwamba kukapendwa na kuchukiwa kwa pale atapoafikiwa katika maneno na vitendo, basi ni katika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi kwa makundi.”[1]

Amesema tena Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah):

“Atakayemfanya mtu miongoni mwa watu – mbali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – yule mwenye kumpenda na kuafikiana naye ndiye katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na yule mwenye kwenda kinyume naye ndiye katika Ahl-ul-Bid´ah wal-Furqah, kama hilo linavyopatikana katika mapote ya wale wafuasi wa maimamu wa wanafasalfa wa dini na wengine, basi huyo ni katika Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal wat-Tafarruq.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (08/20).

[2] Majmuu´-ul-Fataawaa (03/347).

  • Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
  • Imechapishwa: 22/01/2017