Mama wa waumini Umm ´Abdillaah ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuzusha katika amri (yetu hii yale yasiyokuwemo, basi atarudishiwa mwenyewe.”

Hadiyth hii ndio msingi wa Bid´ah kurudishwa katika dini. Matendo yaliyo kwenye dini – yaani mambo ya dini – yamegawanyika:

1-Mambo ya ´ibaadah.

2- Mambo ya mu´amala.

Uzushi unakuwa katika mambo ya ´ibaadah na ya mu´amala. Hadiyth hii inaonyesha dalili ya kubatilisha uzushi na Bid´ah.

“Kila uzushi ni Bid´ah.”

Bi maana kila uzushi katika dini ni Bid´ah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 122
  • Imechapishwa: 17/05/2020