al-Bahrayniy amesema:

“Rabiy´ al-Madkhaliy hakufurishi kwa kuacha “Jins-ul-´Amal”[1]. Anajigonga na anajitahidi kukwepa tamko “Jins-ul-´Amal” kwa madai kwamba Salaf hawakulitumia. Mtu huyu ni mwenye kuchanganya mambo katika masuala ya imani, kitu ambacho hataki kukikubali.” Uk. al-Burkaan, uk. 39

Huu ni uongo mkubwa kabisa. Nimesema mara nyingi kwamba yule asiyefanya matendo yoyote mazuri ni kafiri. Lakini Haddaadiyyah wana msingi mchafu ambao ni kufungamanisha maoni na mtu ambaye hana lolote kuhusiana na maoni hayo na anayakana hadharani. Pamoja na hivyo wanaendelea kumtuhumu kwayo na kuyafungamanisha naye. Kwa msingi huu mchafu wamewapiku hata Khawaarij.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/neno-jins-ul-amal-limetoka-kwa-murji-ah/

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 219
  • Imechapishwa: 09/10/2016