Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kila lililokuja juu ya hayo kutoka katika Hadiyth ambayo ni Swahiyh iliyosimuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi tunaipokea kama alivosema na maana yake ni kama alivokusudia mwenyewe.”

Kila Hadiyth iliyokuja inafasiriwa kama alivotaka Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imaam ash-Shaafi´iy amesema:

“Nimemwamini Allaah na yaliyokuja kutoka Kwake kama alivokusudia. Nimemwamini Mtume wa Allaah na yaliyokuja kutoka kwake kama alivokusudia Mtume wa Allaah.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/265)
  • Imechapishwa: 23/05/2020