Msimamo wako kwa wafuasi wa al-Halabiy


Swali: Vipi tutatangamana na wafuasi wa al-Halabiy Tunisia? Je, tumsuse yule aliyedanganyika naye na akawa ni mmoja katika wao? Ni upi muda wa nasaha?

Jibu: Wafuasi wa al-Halabiy wamegawanyika sehemu mbili:

1- Wale ambao ni washabiki wake na wanajua. Hawa ni kama wao. Kwa kuwa upotevu wa ´Aliy bin Hasan bin ´Abdil-Hamiyd al-Halabiy umeonekana wazi wazi kabisa na sifa mbaya. Ana hoja za udanganyifu. Hayuko kama alivyokuwa akijulikana. Kipindi hichi cha mwisho ´Aliy bin Hasan amechukua njia nyingine tofauti na ile ambayo tulikuwa tunajua akiwemo. Wale ambao ni washabiki wana hukumu moja na yeye.

2- Ama yule aliyedanganyika naye, kama alivyosema muulizaji, huyu anasihiwe. Asisuswe. Anasihiwe na abainishiwe makosa ya watu hawa. Kama Allaah Atakuwa Amemtakia kheri Alhamdulillaah. Na kama bado ataendelea na kushikamana naye basi atachukuliwa kama lile kundi la kwanza baada ya kubainishiwa na kuwekewa wazi na kutajiwa dalili. Akiendelea na msimamo huo huo atachukuliwa ni kama wao.

Ama kuhusu nasaha, haina muda maalum. Unaweza kumnasihi mtu kwenye kikao, vikao viwili, kupitia simu au uandishi. Muhimu ni kwamba mbainishie kosa na upotevu wa mtu huyo kwa dalili na hoja za wazi. Mtu atafahamu. Ana akili. Akikataa anachukuliwa kama wale wengine.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=AMlVvXXl1N4
  • Imechapishwa: 15/05/2018