Msimamo wa waumini na wasiokuwa waumini juu ya ahadi ya Allaah

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

“Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata yale aliyoyaamrisha Allaah kuungwa na wanafanya ufisadi katika ardhi, basi hao ndio waliokula khasara.”

Hapa kunakusanya ahadi ilio baina yao na Yeye na ahadi ilio baina yao na waja Wake aliyowakokotezea nayo kwa maagano imara. Wanapuuza maagano hayo. Bali wanavunja na kuacha maamrisho yake na kukiuka makatazo yake na pia wanavunja maagano yaliyo kati yao na viumbe.

وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ

“… na wanakata yale aliyoyaamrisha Allaah kuungwa… “

Katika haya kunaingia mambo mengi. Hakika Allaah ametuamrisha kuwaunga wale ambao kati yetu sisi na wao tunakutanisha imani na kutekeleza ´ibaadah Yake na wale ambao kati yetu sisi na Mtume Wake tumekutanisha kumwamini, kumpenda, kumnusuru na kumtekelezea haki zake na wale ambao tunakutanisha udugu kati yetu sisi na wazazi wawili, jamaa na marafiki na viumbe wengine. Tunatakiwa kutekeleza haki hizo ambazo Allaah ametuamrisha kuziunga. Waumini wao huunganisha na kuzitekeleza ipasavyo zile haki ambazo Allaah ameamrisha ziunganishwe. Kuhusu watenda madhambi wamezikata na kuzitupa nyuma ya migongo yao na kupingana nazo kwa ufuska, ukataji na ufanyaji maasi ambao ni kule kueneza ufisadi ardhini.

Wale ambao hizo ndio sifa zao basi ni wakhasirikaji duniani na Aakhirah. Khasara imefupika kwao. Kwa sababu khasara yao ni yenye kuenea katika kila hali. Hawana aina yoyote ile ya faida. Kwa sababu sharti ya kila tendo jema ni lazima iwe na imani. Kwa hiyo yule ambaye hana imani basi hayasihi matendo yake. Hapa inahusiana na khasara ya ukafiri. Kuhusu khasara ambayo inaweza kuwa ukafiri, maasi, kuzembea katika kuacha mambo yaliyopendekezwa ambayo imetajwa katika maneno Yake:

إِنَّ الْإِنْسَانَ لَفِي خُسْرٍ

“Hakika mwanadamu yumo khasarani.”[1]

ni khasara yenye kuenea kwa kiumbe wote. Isipokuwa tu yule mwenye kusifika kwa imani, matendo mema, kuuasiana kwa haki na kuusiana kwa subira.

[1] 103:02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 36
  • Imechapishwa: 05/06/2020