Madhara ya tano, ambayo nataraji ndio ya mwisho, naona namna ambavo baadhi ya vijana kazi yao kubwa imekuwa ni kujishughulisha na Anaashiyd pasi na kujali kusikiliza Qur-aan, Hadiyth, barnamiji za kidini za redio, mawaidha, Fiqh na mfano wake. Haya ni majanga na ni viza vilivyopandiana.

Kwa ajili hiyo ni lazima kwa kila kijana wa kiislamu atambue ndani ya moyo wake kwamba kila kheri inapatikana kwa kule kufata na kila shari inapatikana kwa kule kuzua. Muda wa kuwa Maswahabah hawatambui chochote juu ya hayo, basi na sisi hatutakiwi kufanya hivo ijapo baadhi wanafikiria kuwa ndani ya hayo kuna kheri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (158)
  • Imechapishwa: 17/08/2021