Swali: Inajuzu kuwapa salamu wafuasi wa wazushi ikiwa wanafanya ushabiki kwao? Je, inajuzu kuwakata?

Jibu: Kitu cha kwanza ni wajibu kueleza Bid´ah ni kitu gani. Watu wengi ambao wanajinasibisha na kujifunza elimu hii leo kila ambaye anapingana nae kwa kitu basi anamwambia kuwa ni mzushi. Kwa sababu hawajui Bid´ah ni nini. Ni lazima ueleze Bid´ah ni nini. Watu wengi ambao wanajinasibisha na elimu hii leo wanapachika “Bid´ah” juu ya vitu visivyokuwa Bid´ah. Kila ambaye anapingana nae kwa kitu basi wanamwabia kuwa ni mzushi. Hili si sawa na wala haijuzu.

 Bid´ah ni kuzua kitu katika Bid´ah kisichokuwemo. Hivyo ndivyo alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayezua katika amri yetu hii yasiyokuwemo, atarudishiwa mwenyewe.”

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu, atarudishiwa mwenyewe.”

Bid´ah ni kuzua katika dini ´ibaadah ambayo haina dalili katika Qur-aan na Sunnah. Hii ndio Bid´ah. Yule ambaye hali yake ni kama hivyo basi ni mzushi.

Mzushi ni wajibu kwanza kumnasihi, kumlingania kwa Allaah na kumukhofisha juu ya Allaah. Ikiwa kuna mambo yamemtatiza basi anatakiwa kubainishiwa haki. Ikiwa hajadhihirikiwa na kitu vilevile basi anatakiwa kubainishiwa haki na kusimamishiwa dalili. Akiendelea baada ya hapo basi anakuwa mtu wa Bid´ah. Ni wajibu kumkata, kutahadharisha naye na kujitenga naye mbali. Kila mwenye kukubaliana juu ya Bid´ah zake na akamfuata na asipokee nasaha na wala asiachane naye anatakiwa kukatwa kama yeye. Kwa sababu mwenye kukubaliana na mzushi na akaridhia Bid´ah zake basi ni mzushi kama yeye. Katika hali hiyo naye anatakiwa kukatwa kama anavyosuswa mzushi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 08/12/2017