Msimamo wa mwanafunzi kwa wanachuoni


3417- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kula kwenye chombo cha fedha [au dhahabu], hakika anagogomoa tumboni mwake Moto wa Jahannma.”

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (23/388): Ahmad bin Zuhayr at-Tustariy ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Sa´d ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia, kutoka kwa Swaalih bin Kaysaan, kutoka kwa Naafiy´ aliyesimulia kwamba Zayd bin ´Abdillaah alimweleza kwamba ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Bakr alimweleza kwamba Umm Salamah alimsimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

Sababu ya mimi kudurusu vyanzo vya Hadiyth ni kwamba utafiti wangu wa hapo kabla katika ”Irwaa´-ul-Ghaliyl”[1] na ”Ghaayat-ul-Maram”[2] (kupitia kwa Muslim na ziada zengine kati ya vifungu viwili) hakukutajwa uvuaji huu. Pamoja na kwamba as-Suyuutwiy alikuwa ametaja tolea la Muslim la Hadiyth na akanasibisha uvuaji wa at-Twabaraaniy katika kitabu chake ”al-Jaamiy´ as-Swaghiyr”. Wakati nilipotunga kitabu changu ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” nikataja rejea mbili zilizotajwa chini ya Hadiyth na hivi sasa niliporudi kutazama kwa mara nyingine katika toleo langu jipya la ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” na kukagua hizo rejea mbili nikabainikiwa kwamba kunakosekana vyanzo vya Hadiyth zilizoashiriwa hivi sasa na uvuaji wake. Ndio maana nikafanya hivo hivi sasa. Huenda sababu ya mimi kupitwa na hilo ni kwa sababu mjeledi wa sita ambao kuna Hadiyth za Umm Salamah ulikuwa bado haujachapishwa. Ndio maana nikategemea kunyamaza kwa as-Suyuutwiy japokuwa nilijua kuwa kunyamazia kwake ni jambo linahitajia kuangaliwa vizuri sana. Lakini katika hali kama hii hakuna jengine ninaloweza kufanya mimi wala wanafunzi wengine walio kati na kati isipokuwa ni kuwaiga wanachuoni midhali kosa lao halijabainika. Huo ndio mwenendo niliyoenda nao katika tungo zangu zote, khaswakhaswa kwa kuzingatia kwamba uvuaji umetajwa kwa mara zisizodhibitika katika Qur-aan na Sunnah.

[1] Irwaa’-ul-Ghaliyl (1/68).

[2] Ghaayat-ul-Maraam, uk. 75

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/2/1232-1234)