Msimamo wa mwanafunzi kwa mzazi ambaye ni mchawi

Swali: Mtu atahesabika kuwa ni kujitenga mbali iwapo atafichua siri kwenye mihadhara na kuwaeleza watu kuhusu baba ambaye ni mchawi anayedhihirisha mambo ya kishaytwaan pamoja na kuzingatia pia kuwa ameshamnasihi na kumpa mawaidha?

Jibu: Kwa hali yoyote baba – kama mlivyosikia – ana haki juu ya mtoto wake ya kumtendea wema na kumpa matumizi. Miongoni mwa mambo ya wajibu mkubwa kwa mtoto ni kumnasihi baba yake na kumlingania katika dini ya Allaah. Mtazame namna ambavyo Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alivyoanza na baba yake:

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا

“Pindi alipomwambia baba yake: “Ee baba yangu! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote?” 19:42

يَا أَبَتِ

“Ee baba yangu!” 19:43

يَا أَبَتِ

“Ee baba yangu!” 19:45

Ampe nasaha baba yake huenda Allaah akamwongoza. Iwapo atakuwa na wafuasi wenye kupendezwa nae awabainishie na awatahadharishe kutokamana na mchawi huyu na vilevile awabainishie watu ya kwamba ni mpotevu na kwamba ni katika wapenzi wa shaytwaan midhali ataendelea kufuata njia hiyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2044
  • Imechapishwa: 08/10/2016