Msimamo wa Khawaarij na Nawaaswib kwa Maswahabah

Madhehebu ya tatu ni ya Khawaarij na Nawaaswib inapokuja kwa Maswahabah. Madhehebu ya watu hawa ni kinyume na madhehebu ya Raafidhwah ambayo ni kuwachukia watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ahl-ul-Bayt na kuwafanyia uadui.

Wameitwa Nawaaswib kwa kuwa wamejenga uadui kwa Ahl-ul-Bayt.

Wameitwa Khawaarij kwa sababu walimfanyia uasi ´Aliy na wakamfanyia al-Baraa´ baada ya masuala ya hukumu. Hali kadhalika wakamfanyia al-Baraa´ ´Uthmaan baada ya kuwajongeza ndugu zake kwa kuitakidi kwao kuwa amekuwa Faasiq kwa tendo hilo na amemuasi Allaah. Waliosalia katika Maswahabah hawawafanyii al-Baraa´ isipokuwa tu wale ambao wanaonelea kuwa wametenda dhambi kubwa kwa mtazamo wao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/750-751)
  • Imechapishwa: 18/05/2020