Msimamo wa Ibn ´Uthaymiyn juu ya kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa mavazi yaliyo na picha ima ya mnyama au mtu?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kuvaa mavazi yaliyo na picha ya mnyama au mtu. Haijuzu vilevile kuvaa koti, kofia au kitu kingine kilicho na picha ya mtu au mnyama. Hayo ni kwa sababu imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Malaika hawaingii katika nyumba ilio na picha.”

Kwa ajili hii hatuonelei kuwa inafaa kwa yeyote kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu, kama wanavyosema. Yule ambaye yuko na picha kwa ajili ya kumbukumbu basi ni lazima kwake kuichana. Ni mamoja awe ameihifadhi juu kwenye ukuta, albamu au kitu kingine. Kuihifadhi kunapelekea kuwakosesha watu wengine wa nyumbani Malaika kuingia nyumbani mwao. Hadiyth hii tuliyoiashiria imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/166-167)
  • Imechapishwa: 04/06/2017