Msimamo wa Ibn Taymiyyah na Ahl-us-Sunnah juu ya ´Aliy bin Abiy Twaalib


Swali: Kuna kundi la wanafunzi wanoaanza ambao wanasema kuwa Qur-aan imeumbwa na wanadai kuwa Ibn Taymiyyah amemtukana ´Aliy bin Abiy Twaalib – hivi ndivyo alivyosema – katika kitabu chake “Minhaaj-us-Sunnah”. Je, haya ni sahihi?

Jibu: Huu ni uongo na uzushi. Shaykh-ul-Islaam hakumtukana ´Aliy bin Abiy Twaalib. Shaykh-ul-Islaam hakumtukana ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Kinyume chake amesimama upande wake na anampenda. Vilevile anaamini kuwa ni mtoto wa ami yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwamba ni katika watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwamba ni kiongozi wa nne mwongofu na kwamba ni mmoja kati ya wale kumi walioahidiwa Pepo. Haya ndio anayoamini Shaykh-ul-Islaam na Ahl-us-Sunnah wengineo juu ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Hawamchukii na wala hawamtukani. Bali wamesimama upande wake na wanampenda. Huu ni uongo juu ya Shaykh-ul-Islaam na ni uongo vilevile juu ya Ahl-us-Sunnah.

Kusema kuwa Qur-aan imeumbwa ni ukafiri. Kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameeleza kuwa Qur-aan ni maneno Yake na kwamba imeteremshwa kutoka Kwake. Mwenye kusema kuwa Qur-aan ni kiumbe kama viumbe vyengine ni kafiri.

  • Mhusika: Imaam Swalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 19/11/2017