3 – Wanapinga ya kwamba waumini hawatomuona Mola wao siku ya Qiyaamah

Ibaadhiyyah, wakiwa ni wenye kuwafuata viongozi wao Mu´tazilah, wanapinga ya kwamba waumini watamuona Allaah (Ta´ala). Wamefanya hivo kwa kutumia shubuha batili na dhaifu. Wameyathibitisha hayo katika vitabu vyao. Miongoni mwa wa mwisho waliofanya hivo ni yale yaliyotajwa na Muftiy wao al-Khaliyliy katika kitabu chake ”Haqq-ud-Daamigh”. Baada ya kuzitaja Hadiyth kumi na tatu ambazo zote zinathibitisha Kuonekana akasema:

”Mpenzi msomaji! Unaona mwenyewe ya kwamba kuchukua udhahiri wa maandiko haya kunapelekea katika yale yanayorudishwa na akili na kukadhibishwa na dalili.”[1]

Huo ndio msimamo wa imamu na Muftiy wao – anafanya hivo kwa kuwafuata wahenga wenzi – ambapo anarudisha Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutanguliza akili zake mbele ya dalili za Qur-aan na Sunnah. Kuyataja hayo yanatosheleza kumraddi. Vinginevyo mambo ni kwamba waumini kumuona Allaah (´Azza wa Jall) ni jambo limethibiti katika Qur-aan, Sunnah na kupitia maneno ya Salaf wa Ummah huu. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yale waliyomo Salaf wengi ni kwamba yule anayepinga kuonekana kwa Allaah Aakhirah ni kafiri.”

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/aliyosema-al-khaliyliy-juu-ya-udhahiri-wa-maneno-ya-mtume/
  • Mhusika: ´Abdullaah as-Salafiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibaadhwiyyah fiy miyzaan Ahl-is-Sunnah, uk. 19
  • Imechapishwa: 11/02/2017