Wanasema – wafuasi wa Abul-Hasan Ma´ribiy – mwenye madhehebu haya ni al-Albaaniy. Waongo. al-Albaaniy emejitenga mbali [na madhehebu haya]. al-Albaaniy yuko pamoja na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Amepambana kwa ajili ya kuinusuru Manhaj hii. Ameandika vitabu maalum ili kuinusuru Manhaj hii.

al-Albaaniy ni katika Ahl-us-Sunnah juu ya imani ya kwamba mapokezi yaliyopokelewa kwa njia moja yaliyothibiti [Akhbaar-ul-Aahaad] yanafidisha elimu yenye yakini na anaonelea kuwa ni mpotevu mwenye kuonelea kinyume na hivi. Anawasifu kuwa ni Mu´tazilah, Khawaarij na kadhalika. Vipi basi mtu atasema kuwa anakubaliana na Abul-Hasan katika suala hili?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26895
  • Imechapishwa: 20/05/2015