Swali: Nifungamane na ndugu yangu mkubwa ambaye haswali pamoja na kuzingatia kwamba ni ndugu upande wa baba yangu tu?

Jibu: Ambaye anaacha swalah kwa makusudi ni kafiri kufuru kubwa kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni akiwa ni mwenye kukubali uwajibu wake. Akiwa ni mwenye kupinga uwajibu wake ni kafiri kwa mtazamo wa wanazuoni wote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kichwa cha mambo ni Uislamu, nguzo yake ni swalah na jihaad katika njia ya Allaah ndio nundu yake ya juu.”

Ameipokea Imaam Ahmad na at-Tirmidhiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha swalah.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa Sunan kwa cheni ya wapokezi wa Swahiyh.

Jengine ni kwa sababu anayepinga uwajibu wake ni mwenye kumkadhibisha Allaah, Mtume Wake na maafikiano ya waislamu na waumini. Ukafiri wake unakuwa mkubwa zaidi kuliko ukafiri wa anayeacha kwa kuzembea.

Kwa hali zote mbili ni wajibu kwa watawala wa waislamu kuwataka kutubia wale wenye kuacha swalah na vinginevyo wauliwe kutokana na dalili zilizopokelewa juu ya hilo.

Ni wajibu kumsusa mwenye kuacha swalah, kumka na kutoitikia mwaliko wake mpaka atubu kwa Allaah kutokamana na hilo. Sambamba na hilo ni lazima kumnasihi, kumlingania katika haki na kumtahadharisha kutokamana na adhabu inayopelekea kwa anayeacha swalah duniani na Aakhirah. Pengine akatubia kwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/266)
  • Imechapishwa: 05/10/2021