Qur-aal-Marruudhiy amesema:

“Abu ´Abdillaah [Ahmad bin Hanbal] alitwambia: “Adhabu ya kaburi ni haki. Hakuna anayeipinga isipokuwa tu mpotofu na anayepotosha.”

al-Marruudhiy amesema:

“Yule atakayeingilia falsafa hatofaulu. Yule atakayeingilia falsafa hatoiepuka Bid´ah.”

al-Marruudhiy amesema:

“Nilimwambia Abu ´Abdillaah: “al-Karaabisiy anasema: “Yule asiyesema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa ni kafiri.” Akasema: “Bali yeye ndiye kafiri.”

Amesema vilevile:

“Bishr al-Mariysiy alijitokeza na aliyekuja baada yake Husayn al-Karaabisiy. Amekuwa Jahmiy na kuonyesha Jahmiyyah yake. Ni wajibu kutahadhari naye na kila yule anayemfuata.”

al-Khallaal amesema: “al-Marruudhiy alitukhabarisha:

“Abu ´Abdillaah alimtaja Haarith al-Muhaasibiy na akasema: “al-Haarith ndio msingi wa mabalaa yote. Yeye ndiye matatizo. Wengi waliokuwa pamoja naye wamepotea. Isipokuwa tu Ibn-ul-´Allaaf ndiye alikufa hali ya kusitirika. Tahadharishe juu ya al-Haarith kweli kweli!” Nikasema: “Watu wanaenda kwake.” Akasema: “Tunatakiwa kuzungumza nao. Huenda hawatambui Bid´ah yake. Ima wakubali au na wao wasuswe. Haarith hana tawbah. Kila wakati kunatolewa ushuhuda dhidi yake lakini anapinga. Tawbah ni kwa yule anayetambua.”

  • Mhusika: Imaam Abuul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabaqaat-ul-Hanaabilah (1/149-150)
  • Imechapishwa: 10/06/2017