Swali: Naishi katika jamii inayoheshimu desturi za kikabila ambazo mara nyingi zinakuwa ni zenye kupingana na Shari´ah safi. Kama wake wa wanandugu kuchanganyika na ndugu wa waume, kusikiliza nyimbo na mengineyo. Nikiwakataza wananambia kuwa nina msimamo mkali, kwamba nimeleta dini mpya na maneno mengine ya kunikemea. Je, ni haki kwangu kuwasifu kuwa ni mawalii wa shaytwaan? Ni ipi njia nzuri ya kutangamana nao?

Jibu: Njia nzuri ni kuwanasihi, kuwafikishia elimu na kheri na uwe na uvumilivu juu ya yale yatayokufika kutoka kwao. Usikabiliane nao kwa mabaya na maneno maovu. Usifanye hivo. Kabiliana nao kwa upole, usulubu mzuri, hekima, maneno mazuri na ujadiliane nao kwa njia iliokuwa nzuri. Hivyo ndivyo Allaah alivyoamrisha. Kuwa na subira.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (12) http://alfawzan.af.org.sa/node/2055
  • Imechapishwa: 17/03/2017