Msimamo kwa ndugu ambaye anashinda kwenye TV na anaacha swalah za mkusanyiko

Swali: Naishi katika kijiji kilicho mbali na ar-Riyaadh kwa 500 km na naishi pamoja na mjomba wangu. Nyumbani kwetu kuna dishi/king´amuzi. Haendi kuswali swalah ya Fajr pamoja na mkusanyiko. Nimekwishamnasihi juu ya hilo lakini hata hivyo haifui dafu – Allaah amwongoze. Je, niishi mbali na yeye? Nimehisi dhiki kiasi cha kwamba jambo hilo limenishughulisha na kutafuta elimu.

Jibu: Ikiwa hakubali nasaha basi usiingie naye. Lakini kariri nasaha huenda Allaah akamwongoza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 22/03/2019