Swali: Ni vipi unatakiwa kuwa msimamo wetu juu ya Tawraat na Injiyl walivyo navyo mayahudi na manaswara pamoja na upotoshaji unaopatikana ndani yake?

Jibu: Msivikadhibishe na wala msivisadikishe. Kwa sababu kuna uwezekano ndani yake kukawa kuna haki na kukawa pia batili. Sisi Allaah ametutosheleza navyo. Lakini tunasema kuwa vimefutwa na wakati wake umeisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 19/11/2016