Msimamizi wa mwanamke anatakiwa kumsaidia kuhiji

Swali: Je, msimamizi wa mwanamke – mke au msichana – analazimika kumhijisha au atatekeleza hajj pale ambapo zitatimia kwake sharti za hajj?

Jibu: Mwanamke kama ni muweza wa kufanya hajj kwa nafsi yake, mwili wake na pesa zake basi analazimika kufanya hivo. Akiwa hana Mahram basi analazimika kutangamana na Mahram na amhudumie na ampe matumizi ya hajj. Msimamizi wake akiwa ni baba yake basi anatakiwa kuharakisha kumhijisha na amsaidie juu ya faradhi hii. Akiwa sio baba yake, kama vile kaka yake na mfano wake, basi wanalazimika kumcha Allaah na wapupie kumtekelezea dada yao faradhi hii. Wakishindwa kufanya hivo na yeye mwanamke ana uwezo wa kipesa na anaweza kumpa mmoja katika Mahaarim zake ahiji pamoja naye, basi atalazimika kufanya hivo. Jambo muhimu ni kwamba miongoni mwa wema kwa watoto wake wa kike na watoto wake wa kiume ni kuwasaidia kuhiji katika Nyumba tukufu ya Allaah na kutekeleza nguzo hii watapokuwa na uwezo juu ya hilo. Haitakiwi kupuuza si kwa upande wa mume, upande wa msichana huyo, upande wa kaka zake au walezi wake. Wanatakiwa kuharakisha kuhiji wakati kutakapotimia zile sababu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-ولي-الأمر-ملزم-بتحجيج-المرأة
  • Imechapishwa: 11/06/2022