Swali: Kuna baadhi ya misikiti sehemu ya kuswalia kunakuwa ni kwenye ghorofa ya pili na chini yake kwenye ghorofa ya kwanza kunakuwa ni vyoo. Ni ipi hukumu ya kuswali katika misikiti kama hii?

Jibu: Hakuna neno. Maadamu kuna sakafu kati yake inayotenganisha vyoo, hakuna neno. Kadhalika hakuna neno kuswali juu ya kifuniko cha kisima kwa kuwa kuna kizuzi baina yako wewe na taka. Bali wanachuoni wanasema swalah ni sahihi, au imechukizwa, mtu akiswali sehemu kuliko najisi kukiwa kumefunikwa na udongo au mkeka. Ikiwa hakuna nafasi na msikiti ukalazimika kujengwa juu ya vyoo au kukawa na haja watu kuswali juu ya kifuniko cha kisima, ni kama tulivyosema hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 10/04/2017