Msichana wa miaka 13 amepitwa na siku 7 za Ramadhaan

Swali: Mimi ni msichana ambaye nina miaka kumi na tatu. Nilikula katika Ramadhaan siku saba kwa sababu ya ujinga. Ni kipi kinachonilazimu hivi sasa?

Jibu: Akichelewa [kulipa] zaidi ya mwaka mmoja basi bora kwake ni yeye kulisha juu ya kila siku moja masikini. Ama ikiwa bado hajabaleghe kwa njia ya kwamba ima hajaanza kupata hedhi, hazijaota nywele za sehemu za siri wala kwapani na hajaanza kuota na kumwaga, basi anazingatiwa kwamba bado hajabaleghe. Katika hali hiyo sio wajibu kulipa. Ama akiwa amekwishabaleghe basi ni wajibu kwake kulipa pamoja vilevile na kutubu, kuomba msamaha na kulisha akiwa ni muweza wa kufanya hivo kwa njia ya usalama zaidi. Hivyo ndivo walivyofutu kundi la Maswahabah. Chakula kusuduwa ni takriban 1,5 kg katika kile chakula kinacholiwa zaidi katika mji. Hapa ni pale atapokuwa ni muweza. Akiwa si muweza basi itakuwa sio wajibu kwake kulisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 28/10/2018