Msichana anatakiwa kupigwa mawe kwenye mlango wa nyumba ya baba yake katika Biblia


13Ikiwa mtu atamuoa mwanamke na baada ya kufanya naye tendo la ndoa, akamchukia, 14akimsingizia na kumwita jina baya: ”Akasema, “Nilimuoa mwanamke huyu, lakini nilipolala naye sikupata uthibitisho wa ubikira wake”, 15basi hapo baba na mama wa msichana wataleta uthibitisho kwamba alikuwa bikira kwa wazee wa mji kwenye lango. 16Baba wa msichana atawaambia wazee: ”Nilimuoza binti yangu kwa huyu mwanaume, lakini hampendi, 17sasa amemsingizia na kusema kwamba hakumkuta binti huyu akiwa bikira. Lakini uthibitisho huu hapa wa ubikira wa binti yangu.” Kisha wazazi wake wataonyesha nguo zake kwa wazee wa mji, 18na wazee watamchukua huyo mwanaume na kumuadhibu na 19watamtoza shekeli mia moja za fedha na kupewa wazazi wa msichana, kwa sababu mwanaume huyu amempa bikira wa kiisraeli jina baya. Ataendelea kuwa mke wake, kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake. 20Hata hivyo, ikiwa tuhuma hizo ni za kweli na hakuna uthibitisho juu ya ubikira wa huyo msichana ulioweza kupatikana, 21huyo msichana atatakiwa kuletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe, kwa sababu amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kutokuwa na utaratibu wakati akiwa nyumbani kwa baba yake. Mnatakiwa muondoe uovu katikati yenu.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kumbukumbu la torati 22:13-21
  • Imechapishwa: 27/10/2017