Mshirikina kupokelewa maombi yake sio hoja ya aliyomo

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Aliitikia (Du´aa ya) Bal´am bin Baa´uur juu ya watu wa Muusa ambao wao walikuwa ni waumini na Allaah Akawasibu na majanga.”

Miongoni mwa mambo ambayo yanayotolea dalili kuonesha kuwa mmoja wao – yaani waabudu makaburi na washirikina – wanapoomba kwenye masanamu yao, kwenye kaburi au akimuomba maiti anaweza kuitikiwa, hii haijakuwa ni dalili ya usahihi wa aliyomo. Huyu Bal´am ni katika wanachuoni wa Banuu Israaiyl na alikuwa ni mtu ambaye anaitikiwa Du´aa zake. Muusa aliwapiga vita makafiri na yeye huyo mwanachuoni alikuwa miongoni mwao. Wakamtaka aombe dhidi ya Muusa na watu wake ila akawa amekataa. Kisha wakamng´ang´ania mpaka akawa ameomba dhidi ya Muusa na watu wake. Wakati huo ndipo Allaah Akawa amemuadhibu Muusa na watu wake. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا

“Na wasomee habari za yule ambaye Tulimpa (ujuzi wa) Aayah Zetu akajivua nazo (asizifuate), na shaytwaan akamfuata na akawa miongoni mwa waliopotoka. Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayah), lakini aligandamana na dunia (kutaka anasa na ukubwa) na akafuata hawaa yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu atahema (na kuning’iniza ulimi nje) na ukimwacha pia atahema. Hivyo ndiyo mfano wa watu waliokadhibisha Aayah Zetu.” (07:175)

Hichi ndio kisha cha Bal´am Allaah Amekitaja katika Qur-aan. Wakati ambapo hakuitendea kazi elimu yake na akaomba dhidi ya Muusa na watu wake na Allaah Akawa amemuitikia Du´aa yake, hii bado haijakuwa dalili ya kuonesha usahihi wa aliyomo wala usahihi wa aliyoyafanya. Haya ni majaribio kwake.

Anaendelea kusema (Rahimahu Allaah):

“Washirikina pia wanaweza kuomba kunyeshelezewa wakanyeshelezewa, wakaomba kunusuriwa na wakanusuriwa”

Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ

“Au Yule Anayemuitika aliyedhikika anapomwomba, na Akamuondoshea dhiki… “ (27:62)

وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ

“Na inapokuguseni dhara baharini hupotea wale mnaowaomba (hamuwaiti wakati huo wa shida) isipokuwa (mnamwita na kumuomba Allaah) Yeye Pekee.” (17:67)

Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anawaitikia washirikina ilihali ni washirikina wakati ambapo wanamuomba katika hali ya dharurah. Hii sio dalili ya kusihi yale waliyomo katika kufuru na shirki, bali kule kuwaitikia ni Rahmah kwao vile wamemuomba katika hali ya dharurah na wakamtakasia Du´aa na hawakumuomba Yeye pamoja na wengine katika hali hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2245
  • Imechapishwa: 05/05/2015