Mshirikina, al-Jifriy, ambaye anatambulikana kwa ushirikina wake wa wazi, amesema:

“Nawapa changamoto hawa ambao wanatuharamishia kumwaudu Allaah kupitia waja Wake wema. Kwa sababu Allaah ametuwekea katika Shari´ah kumwabudu kupitia viumbe visivyokuwa na uhai. Vipi basi tusimwabudu Allaah kupitia waja Wake wema?”

Kivipi, ee mshirikina al-Jifriy? Anasema kuwa Allaah ametuwekea Shari´ah ya kutufu kwenye Ka´bah. Huku si ni kufanya ´ibaadah kupitia kiumbe kisichokuwa na uhai? Allaah ametuwekea Shari´ah ya kulala Minaa, kusimama ´Arafah, kulala Muzdalifah na kurusha vijiwe kwenye kiguzo. Je, huyu kweli anafahamu nembo [za ´ibaadah]? Hafahamu nembo. Vinginevyo angeliyasema yale yaliyosemwa na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) kuhusu jiwe jeusi:

“Mimi najua si vinginevyo wewe ni jiwe tu ambalo hudhuru na wala hunufaishi. Laiti si kumuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikubusu basi nami nisingekubusu.”

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=dDamOTOimh8
  • Imechapishwa: 06/09/2020