Msalaba katika michezo ya watoto

Swali: Kwenye kompyuta kuna michezo ambayo wakati mwingine kunaonekana misalaba. Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Nasaha zangu ni zile nilizoashiria punde kidogo; kwamba ni wajibu kuiharibu misalaba au kuivunja ikiwa haiwezekani kuiharibu. Tambua kwamba mtoto mdogo akizowea kutazama msalaba na akawa mara kwa mara anautazama basi atauchukulia wepesi.

Kwa hivyo ni wajibu kwetu kuwaepusha watoto wetu na kila kitu chenye msalaba. Ni mamoja vile vitu wanavyoona kwenye kompyuta au kwenye magari madogo ambayo wanacheza nayo watoto. Baadhi yake yanakuwa na misalaba ima pembezoni mwake au nyuma yake. Yote haya ni wajibu kwetu kuwaepusha kwayo watoto wetu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1105
  • Imechapishwa: 08/04/2019