Msafiri wa siku tatu anaruhusiwa kutofunga?

Swali: Nikiwa msafiri na nimepanga kukaa siku tatu inafaa kwangu kula safarini?

Jibu: Ukiwa msafiri basi inafaa kwako kula katikati ya safari yako na katika ile nchi utakayokaa. Kwa mfano utaenda Makkah kwa ajili ya kufanya ´umrah kwa siku tano au sita, utakula huko Makkah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoufungua mji wa Makkah katika mwaka wa nane baada ya kuhajiri tarehe 18 au 21 Ramadhaan ambapo akala siku zilizobaki za mwezi na wala hakufunga. Bali alikuwa anakula na anakunywa na anafupisha swalah. Inafaa kwako kula Makkah wakati wa safari yako hata kama hakuna ugumu katika kufunga. Lakini bora ni wewe kufunga ikiwa hakuna ugumu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/134)
  • Imechapishwa: 22/06/2017