Msafiri wa siku mbili anatendea ruhusa za usafiri?

Swali:Kuna mtu kasafiri katika mji kwa muda wa siku mbili. Je ale kwa muda wa siku mbili kama jinsi anavyofupisha swalah kwa kuwa ni msafiri, au kula inakuwa ni khaswa njiani tu?

Jibu: Ninavyoona ni kuwa anachukua ruhusa kama za msafiri. Msafiri akifika katika mji akakaa siku moja, mbili, tatu mpaka siku nne anachukua ruhusa za msafiri. Miongoni mwazo ni kula, na ikiwa atafunga kwa khiyari yake ni khayr kwake.  Ama kujumuisha swalah asijumuishe hilo linakuwa wakati wa haja tu. Akihitajia atajumuisha la sivyo kila faradhi ataiswali kwa wakati wake. Kufupisha anaweza kufupisha isipokuwa tu akiswali nyuma ya imaam mkazi hapo ataswali swalah kikamilifu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020