Swali: Mfungaji akiwa ndani ya ndege na anatazama saa na simu ili apate kufuturu kwa mujibu wa nchi ilio karibu naye – inafaa kwake kufanya hivo pamoja na kuzingatia kwamba anaona jua kwa sababu ndege kuwa juu sana? Ni ipi hukumu ikiwa atakata swawm na pindi ndege ilipopanda juu akaliona jua?

Jibu: Ikiwa mfungaji yuko ndani ya ndege na anatazama saa na simu juu ya ukataji funga wa nchi ilio karibu naye na wakati huohuo analiona jua kwa sababu ya ndege kuwa juu, basi haifai kwake kukata swawm. Kwa sababu Allaah amesema:

ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

”Kisha timizeni funga mpaka usiku.” (02:187)

Hiki ndio kidhibiti kinachomgusa na yeye muda wa kuwa analiona jua. Akifungua na nchi fulani baada ya kumalizika mchana wao na ndege ikaanza safari kisha akaliona jua, basi atatakiwa kuendelea kula. Kwa sababu hukumu yake ni ile ya mji alikotoka na mchana umemalizika akiwa katika mji huo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (1693)
  • Imechapishwa: 24/04/2020