Msafiri na swalah ya ´Iyd


Swali: Je, swalah ya ´Iyd imewekwa katika Shari´ah kwa yule ambaye ni msafiri?

Jibu: Swalah ya ´Iyd haikuwekwa katika Shari´ah kwa msafiri kama ambavo vilevile swalah ya ijumaa haikuwekwa katika Shari´ah kwa msafiri. Lakini msafiri akiwa katika katika mji ambapo kunaswaliwa swalah ya ´Iyd basi anatakiwa kuamrishwa kuswali pamoja na waislamu wenzake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/236)
  • Imechapishwa: 14/06/2018