Msafiri kuswali ´Ishaa kabla ya wakati wake


Swali: Msafiri ameswali Maghrib kwa wakati wake, kisha baada ya nusu saa kabla ya kuingia wakati wa ´Ishaa akasimama na kuswali swalah ya ´Ishaa kwa kufupisha. Ni ipi hukumu ya kitendo chake hichi?

Jibu: Hili ni kosa. Huku inakuwa sio kujumuisha tena. Kujumuisha ni lazima swalah mbili ziwe zimekamatana na baina yake iwe muda mfupi kama wa kiasi cha kutia Wudhuu´ na mfano wa hayo. Ama kukishapita muda mrefu kujumuisha kunabatilika. Kujumuisha kunashurutisha kufuatanisha. Aicheleweshe mpaka itapoingia wakati wake na aiswali ´Ishaa kwa wakati wake kwa kuwa kujumuisha kumempita. 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (62) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13740
  • Imechapishwa: 16/11/2014