Msafiri kula Ramadhaan kabla ya kuanza safari

Swali: Je, inajuzu kwa mtu aliyenuia safari kula kabla hajatoka nyumbani kwake? Ikiwa inajuzu ni ipi hukumu ikiwa atanuia safari na akala kabla ya kutoka halafu asisafiri tena?

Jibu: Haijuzu kwa mwenye kunuia safari kula mpaka atoke katika mji. Hilo ni kwa kuwa rukhusa za safari zimefungamana na kupatikana kwa safari kimatendo. Kwa kuwa Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ

“Mtakaposafiri katika ardhi, basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah.” (04:101)

Amesema “mtakaposafiri” na Hakusema “mtakapotaka”. Neno “kusafiri” inakuwa kwa kutoka katika mji. Haijuzu kwa anayenuia safari kula isipokuwa mpaka pale ataposafiri kimatendo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 23/09/2020