Swali: Kukiadhiniwa swalah ya Dhuhr na bado niko katika mji, kisha nikatoka kwenye manyumba naelekea safari na nikaswali Dhuhr kikamilifu, je, inajuzu kwangu kujumuisha na ´Aswr na nikaifupisha?
Jibu: Ndio, hakuna neno. Hakuna neno ukajumuisha ´Aswr pamoja na Dhuhr ambayo umeiswali kikamilifu kwa vile imekuwajibikia ukiwa bado ndani ya mji wako.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-02-09.mp3
- Imechapishwa: 11/11/2014