Swali: Msafiri akila wakati wa safari yake, je, ni lazima kwake kujizuia akifika katika mji wake katikati ya mchana na ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Bila ya shaka. Ni lazima kwake kujizuia kwa kuwa kula kumefungamanishwa na safari na safari imekwisha. Safari imekwisha. Anatakiwa kujizuia siku iliyobaki kwa kuheshimu wakati. Kwa kuwa safari imekwisha. Hukumu inakwenda na ila yake, inapokuwa na inapokosekana. Pamoja na kujizuia huku anatakiwa siku hii kuilipa kwa kuwa hakuifunga kikamilifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-02-09.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014