Msafiri anataka kufupisha nyuma ya imamu ambaye ni mkazi


Swali: Je, inafaa kwa msafiri kutoa Tasliym pamoja na imamu pindi atapojiunga na imamu ambaye ni mkazi katika zile Rak´ah mbili za mwisho na huku akinuia kufupisha swalah?

Jibu: Haijuzu kwa msafiri atapoongozwa katika swalah na ambaye ni mkazi kufupisha swalah kutokana na ujumla wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yale mtakayowahi swalini na yale yaliyokupiteni kamilisheni.”

Kujengea juu ya hili pindi msafiri atapojiunga pamoja na imamu ambaye ni mkazi katika zile Rak´ah mbili za mwisho basi ni wajibu kwake kukamilisha Rak´ah mbili zengine baada ya imamu kutoa salamu. Haijuzu kwake kutoa salamu pamoja na imamu kwa kufupika kwa hizo Rak´ah mbili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/453)
  • Imechapishwa: 05/08/2017