532- Nilimsikia Ahmad bin Hanbal akiulizwa juu ya mtu ambaye anaswali juu ya meli kwa kukaa. Akasema:
“Ikiwa alikuwa anaweza kuswali kwa kusimama, basi naonelea kuwa airudi swalah yake.”
533- Nilimsikia Ahmad bin Hanbal akiulizwa juu ya mtu ambaye anaswali juu ya meli ambapo akajibu kwa kusema:
“Aswali kwa kusimama iwapo anaweza kufanya hivo.”
- Mhusika: Imaam Abu Daawuud as-Sijistaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 110
- Imechapishwa: 06/07/2019