Msafiri anajiunga na mkusanyiko bila ya kujua hali ya imamu

Swali: Kuna msafiri ameingia msikitini na akaswali pamoja na mkusanyiko Rak´ah mbili. Halafu imamu akatoa salamu na yeye hajui kama watu hao ni wasafiri au wakazi. Je, akamilishe swalah yake au aifupishe?

Jibu: Atazame vile viashirio vya hali. Ikiwa uko katika msikiti ambao wanaswali ndani yake wasafiri, kwa mfano misikiti ilioko katika wanja za ndege, mara nyingi wanaoswali ndani yake ni wasafiri. Hivyo ifanye swalah yako ni kama ya wasafiri. Ama ukiwa ndani ya nchi, basi inatambulika kuwa misikiti ya ndani ya mji wanaoswali ndani yake ni wakazi. Hivyo kamilisha swalah yako Rak´ah nne. Ukiwa na mashaka basi lililo salama zaidi ni wewe kuswali Rak´ah nne kwa sababu haikudhuru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1307
  • Imechapishwa: 25/10/2019